Jumatano, 9 Desemba 2015
Jumanne, 10 Novemba 2015
MHAZINI WA KANISA NDG:SAMORA KIBOYE AFANYIWA OPERESHENI
Mhazini wa kanisa la shirati central sda ndgu samora kiboye amelazwa katika hospitali ya KMT KABWANA hospitali ya wilaya ya rorya .mhazini huyo wa kanisa mwenye umri wa miaka 35 alianza kuumwa kuanzia 07/11/2015 akiwa dukani kwake mda wa saa 3:00 asubuhi ndipo alipoanza kuhisi maumivu tumboni ilipo fika majira ya saa nne usiku alizidiwa na kufikishwa hospitalini baada ya kupimwa na kugundulika kuwa ana APENDEX na madktari kuamua kumfanyia operesheni 10/11/2015 mda wa saa 5 asubuhi ndgu samora kiboye bado yupo chini ya uangalizi wa madktari hadi pale atakaporuhusiwa tuzidi kumuombea
Ijumaa, 30 Oktoba 2015
WASILIANA NA KANISA
wasiliana na kanisa kwa
E MAIL ADRESS shiraticentralsda@gmail.co
BOX 198 SHIRATI RORYA
E MAIL ADRESS shiraticentralsda@gmail.co
BOX 198 SHIRATI RORYA
KANISA YAOMBA AMANI NCHI NZIMA
Kanisa la wasabato la shirati central iliyoko shirati Rorya Mara inapenda kuwapongeza watanzania wote waliyoshiriki uchaguzi wa nchi huku likiomba kwa dhati kabisa Amani kuwepo ndani ya nchi kwani muweza yote ni Mungu ambaye yy ndiye alimuumba kila mwanadamu hata kama aliyeteuliwa kuwa mkuu wa nchi yetu hakuwa chaguo lako lkini tumuombe tu muumbaji wetu Tanzania izidi kuwa na amani na aliyeteuliwa atende kazi huku Mungu akitanguliza fimbo yake mbele yake ili tusiingie ktkt taabu yoyote ktk nchi yetu ndani ya miaka yote mitano ktk uongozi wake wote ndani ya miaka mitano
TUIOMBEE UCHAGUZI WA KANISA
Wapendwa tuendelee kuiombea kanisa kwani tarehe 1/11/2015 siku ya jumapilii kanisa la shirati central litakuwa na uchaguzi wa watendakazi wa mwaka 2016 Tuzidi kumuomba Mungu achague viongozi wa kanisa wajumbe wa baraza la uchaguzi watumike kama chombo tu. MUngu akubariki saana
Jumapili, 4 Oktoba 2015
TAZAMA UKURASA HUU KUSOMA MUHTASARI MUHIMU WA LESONI KWA AJILI A WIKI HII
SIKU SOMO
jumapili Historia ya haraka. waamuzi .{2:1-15} ni nni kilichosababisha zahamahii ns ilidhihirishwaje?
Jumatatu------------------------------------------------------Falme mbili:1wafalme12:26-31 je hili linapaswa kutuambia nini namna ambavyo hali ya mambo iliyopo inaweza kupofusha uamuzi wetu kiasi hicho?
Jumanne--------------------------------------------------Maovu mawili:yeremia 2:1-8, soma haya hii yote
Jumatano------------------------------------------------------Tishio la Bbabeli:yere 27:6,yeremia 25:8-12 Ujumbe wa yeremia kwa watu wa yuda ulikuwa upi?
Alhamisi------------------------------------------------Kuapa kwa Uongo;yeremia 5:1,yr 5:2,3 tazama pia law 19:12 Ni mambo gani yanazungumziwa hapa?
ijumaaa JIFUNZE ZAIDI
SOMO LA WIKI HII:ZAHAMA {Ndani na Nje}
soma mafungu haya kwa ajili ya juma hili:Amu 2:1-15,1wafalme 12:26-31 2nyaraka33:9,10:yeremia 2:1-28 5:2,3
FUngu la kukariri Israel walikuwa utakatifu kwa Bwana,malimbuko ya uzao wake:wote watakaomla watakua na Hatia,uovu utawajalia:asema Bwana{Yeremia 2:3
FUngu la kukariri Israel walikuwa utakatifu kwa Bwana,malimbuko ya uzao wake:wote watakaomla watakua na Hatia,uovu utawajalia:asema Bwana{Yeremia 2:3
Jumamosi, 3 Oktoba 2015
HIVI NDIVYO SABATO YA KWANZA YA 03\10\2015 ILIVYOANZA
HATIMAYE ROBO YA NNE imeanza rasmi na katika sabato hii ya kwanza iliyoambatana na ibada ya maombi ya kufunga kilianza na mkutano wa waalimu kwa kujifunza mwongozo wa kujifunza biblia(LEASONI> Na baadae muda wa kuimba nyimbo za kikristo ilifuatia kabla ya huduma kuu
Ijumaa, 2 Oktoba 2015
SOMA MWONGOZO WA KUJIFUNZA BIBLIA KILA SIKU
Bofya hapa ujisomee lesoni yako kila siku katika page yetu hii.
Ndugu msomaji wa mwongozo wa kujifunza biblia usije ukakosa kusoma lesoni ya robo hii ambayo masomo yote tutakuandalia na kusoma online kupitia website yetu hii
Jumamosi, 26 Septemba 2015
KARIBUNI KWENYE KANGAMANO LA KWAYA
Karibuni kwenye kongamano la kwaya litakalofanyika rasmi katika eneo la kanisa la SHIRATI CENTRAL siku ya jumapili tarehe 27/9/2015 kuanzia saa mbili kamili asubuhi.Kwaya lengwa ni Shirati central
Shirati east
Obwere
Bwiri
Mbire
kinyence
kabwana
sidika
sota
minigo
Ryagati
bunyangi na mengineyo
Kwaya hizi zote zinatoka katika mitaa miwili yaani VICTORIA na SHIRATI njoo ushuhudie mwenyewe waimbaji wakimwimbia Mungu bila hofu na sauti zenye kusikika za kubariki.
Njoo hubarikiwe mpendwa
Ijumaa, 28 Agosti 2015
JINA LINALOOGOPWA NA WENGI.bofya hapa ujue
Katika maisha yako yote jina gani unaliogopa zaidi?
hilo lilikuwa ni swali ngumu katika ibada hii ya leo ndani ya kanisa la shirati central
soma MATENDO YA MITUME 4:12 uangalie jina lenye faida zaidi kwa watu na linaloogopwa
soma KUTOKA 15:......utazame namna ambavyo Mungu alimshughulikia Farao
mpendwa msomaji tafadhali fatilia mafungu hayo utagundua jina linalohitajika kuogopwa na kuinuliwa watu wote ktk ulimwengu huu
Ijumaa, 14 Agosti 2015
Alhamisi, 13 Agosti 2015
HEBU ZITAMBUE SIRI ZILIZOPO KWENYE NAMBA MBALIMBALI KUHUSU MAMBO YA KIROHO
/ZIJUE NAMBA\
Mwanzo 6;14
1korintho2;10 ufunuo 19;10
No 1,maana yake
@Mungu ni mmoja, kumbukumbu la torati 6;4
B,kanisa ni
moja}efeso 4;4
C,iman ni moja}efeso
4;4
D,ubatizo ni moja efeso 4;4-6,1 korintho 12;13
NO 2,Maana yake kiunabii ktk biblia
@Agano la kale na agano jipya{mathayo 13;31-52
B,watu wawili{mwanamke na mwanaume}kuunganshwa na kuwa mwili
mmoja;Mathayo 19;3-6
NO 3 Maana yake:Ushirika wa utatu mtakatfu yaani Mungu
baba,mwana na Roho mtakatifu
1 Yohana 5:8
Mwanzo 1:26
2 Korintho 13:14
No4: Maana yake katika biblia
A: Pande nne za dunia
B: Malaika walioshika pande kuu za dunia ili shetani
asidhuru dunia mpaka mungu amalze kupiga muhuri wa watu wake Daniel 7:1-2,
Ufunuo7:1-3
No7: Ukamilifu wa mungu(siku sita fanya kazi yake)
Ufunuo 6:1,ufunuo 8:1,8:6,ufunuo 1:20,ufunuo10:3
No 12:Ufunuo21:9-24,ufunuo 21:21
No 24:A:Viti vya ukuhani
B:Viti 24
vinakaliwa na watu 24 ufunuo 4:1-10,Mathayo 27:51
No 30:Ukomavu wa kikohani luka 3:23
No40:Uzoefu wa mambo ya kiroho luka 4:1
Mwanzo 7:17,Mathayo3:1,Yohana 3:1
No 50:Jubeled(mambo ya walawi 25:10
No300:Ushuhuda wa Gidioni Waamuzi 7:19,Ufunuo 17:13
KUNENA KWA LUGHA:
TUNAWEZA KUMTAMBUA
MTU AMBAYE ANANENA KWA ROHO?
1:Lazima aweze kufasiri baada ya kunena
2:Lazima mtu asiye wa kabila lake amuelewe
3:Lazima awe amebatizwa kwa roho kama kristo alivyosema.
1Wakorintho 14:6-9
maana kuna lugha nyingi duniani lakini
je kama hakuna roho mtakatifu je twayaweza kuyasikia?
SWALI:Je mtu asiyeweza kufasiri alichokinena anaongozwa
na roho?
1Wakorintho 14:10-15 Basi
ikiwa tunanena kwa roho tuombe tupewe kufasiri lakini kama huwezi kufasiri basi
hujui ulinenalo.
Matendo ya mitume 2:1-12 Siku ya pentekosti
wanafunzi walinena kwa roho na hata watu wote wakaelewana.
Mathayo 3:11-12 yeye awabatizaye kwa roho
na moto ndiye muweza yote yesu kristo
Je lugha unayoisikia ikinenwa na waganga wachawi na wengine
unaisikia?.
Kubali kumpokea kristo ili upate kufunuliwa habari hizi ZABURI 25:14 Siri yake ameificha kwa wale
wamchao tu.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)















